RC HAPI AKUTANA NA WAZEE WA MKOA WA IRINGA, ASIMIKWA RASMI KUWA CHIFU WA WAHEHE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC HAPI AKUTANA NA WAZEE WA MKOA WA IRINGA, ASIMIKWA RASMI KUWA CHIFU WA WAHEHE

 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Ally Salum Hapi leo amefanya mkutano na wazee wa Mkoa wa Iringa ambapo wamemsimika rasmi kuwa Chifu wa wahehe, kama ishara ya kumpokea na kumpa nguvu ya kutawala mkoa wa IRINGA.
Katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa siasa ni Kilimo, wazee wa Iringa wamejitokeza kwa wingi kiasi cha wengine kukosa nafasi ya kukaa na hivyo kusimama na wengine mamia kuketi nje ya ukumbi huo.
RC Hapi alianza kwa kuwapa salamu za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli na baadae kutoa hotuba ya dira ya uongozi wake mkoani Iringa, vipaumbele vyake na kuwaomba ushirikiano wananchi wa Iringa.
"Mhe Rais amenituma niwape salamu zake. Lakini pia amenipa kazi ya kuhakikisha tunawatumikia na kutatua kero zenu ili wana Iringa mjivunie kuwa hamkukosea kumchagua Rais Magufuli na mjisikie fahari na nchi yenu. Siku zote nitasimama upande wenu wananchi na hasa wanyonge..."Alisema Hapi
Katika hatua nyingine RC Hapi alitoa fursa wazee hao kueleza matarajio yao na changamoto zao am... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More