RC KIGOMA ATOA ONYO KWA WEZI WA MIUNDOMBINU YA SERIKALI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC KIGOMA ATOA ONYO KWA WEZI WA MIUNDOMBINU YA SERIKALI


Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga amewataka vijana mkoani Kigoma kuacha wizi wa miundombinu ya Serikali na kwa atakayekamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Hayo aliyasema leo wakati wa uzinduzi wa Sanamu ya Samaki aina ya Mgebuka ambapo alisema kumekuwa na tabia ya vijana wengi kuiba taa za barabarani na wengine kuvamia majimbani na kuiba, na kuwataka waache tabia hiyo na kufanya kazi.

Aidha Mkuu huyo alisema kuanzia sasa wafanyabiashara mkoani Kigoma waanze kufanya hadi saa sita usiku tofauti na mwanzo ambapo walikuwa wakifunga maduka yao saa kumi na mbili jioni kwa kuwa ulinzi umeboreshwa mkoani Kigoma na Miundombinu imeboresha kwa kuwa Serikali imejipanga kuwasaidia Wananchi kuleta maendeleo.

Alisema Kwa yeyeto atakayekamatwa akijihusisha na ujambazi hawatamvumilia, na kutoa onyo kwa kikundi cha vijana kinacho jishughulisha na masuala ya ubakaji na wizi kuacha maramoja na endapo watakamatwa s... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More