RC Kigoma: Bodi ya Mikopo mnafanya kazi kubwa - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC Kigoma: Bodi ya Mikopo mnafanya kazi kubwa

*Aagiza taasisi zinazodaiwa malimbikizo kulipa mara moja 
Na Eline Maronga – HESLB, Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali (mstaafu) Emmanuel Maganga amewaagiza waajiri wote mkoani Kigoma ambao wanadaiwa malimbikizo ya makato ya mikopo ya elimu ya juu kuhakikisha wanawasilisha fedha hizo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) mara moja.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa maagizo hayo Jumanne, Machi 12, jioni wakati akikabidhi tuzo zilizotolewa na HESLB kwa waajiri watano bora mkoani Kigoma ambao wanatekeleza matakwa ya sheria ya HESLB kwa ufanisi.
“Nawapongezeni sana Bodi ya Mikopo, mnafanya kazi kubwa sana kwa taifa letu. Lakini nimeambiwa kuna baadhi ya taasisi hapa mkoani kwangu zinawakata wafanyakazi lakini hazileti kwenu fedha za makato, nimeshaelekeza wahakikishe fedha hizo zinalipwa mara moja,” alisema Brigedia Jenerali Maganga.
Kiongozi huyo, ambaye alikua mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Lake Tanganyika, aliihimiza Bodi ya Mikopo ku... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More