RC MAKONDA AFUTURISHA MAMIA YA WANANCHI DAR, AOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC MAKONDA AFUTURISHA MAMIA YA WANANCHI DAR, AOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI

Na Said Mwishehe, Globu ya jamiiMKUU wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba viongozi wa dini kuendelea kumuombea Rais Dk.John Magufuli kwani anafanya kazi ngumu na kitu pekee ni kuendelea kumuombea. Amesema kwa nafasi ya Rais wapo ambao wanampenda na wapo ambao wanakasirishwa lakini cha msingi ni kuongeza maombi na Dia kwa Rais wetu huku akihimiza umoja na mshikamano. Makonda ametoa kauli hiyo leo jioni hii katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam kabla ya futari maalum ambayo ameiandaa kwa mamia ya wakazi wa Mkoa huo. Amesema viongozi wa dini wana nguvu kubwa na ndio maana watu wanakwenda Kanisani, watu wanakwenda Msikiti na kueleza nguvu hiyo itumike kushirikiana na Serikali. Hivyo ameomba viongozi wa dini kuendelea kumuombea Rais Dk.John Magufuli ili aweze kulitumikia Taifa na kusisitiza nafasi anayoitumikia Rais ni kubwa na inahitaji maombi. 
"Rais wetu anafanya kazi kubwa, na dua za viongozi wa dini ni muhimu ili aweze kulitumikia vema taifa letu. Kam... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More