RC MAKONDA ATANGAZA ZAWADI NONO KWA WADAU WA MITANDAO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC MAKONDA ATANGAZA ZAWADI NONO KWA WADAU WA MITANDAO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Julai 11 ametangaza Shindano litakakalohusisha Watu wote wanaoendesha Platform za Social Media ikiwemo Waandishi wa habari Blog, Website, Online Tv, Instagram, Twitter, Facebook na nyinginezo ambapo watakuwa na jukumu la kuuliza wananchi maswali kuhusu Jumuiya ya Nchi za SADC ambapo washindi wa shindano hilo watajishindia kitita cha mamilioni ya Fedha.
RC Makonda amesema utaratibu wa kushiriki Shindano hilo ni Wahusika kwende kwenye sehemu za Bar,Saloon,Vijiwe vya bodaboda na Sokoni kisha kuwahoji wananchi waeleze namna wanavyoifahamu jumuiya ya SADC na kurusha mahojiano hayo kwenye platform zao ambapo pia wananchi watakaoweza kutoa majibu kwa ufasaha nao watapatiwa kiasi cha shilingi Laki moja.
Aidha RC Makonda amesema Mshindi wa kwanza wa shindano hilo atapatiwa kiasi cha Shilingi Milioni 3, Mshindi wa pili Milioni 2 na Mshindi wa tatu Milioni 1 ambapo hafla ya kukabidhi zawadi hizo itafanyika August 05 mwaka huu.
Hata hivyo RC Makonda... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More