RC MAKONDA ATOA SIKU 30 KWA KAMPUNI YA NYANZA KUMALIZA MIRADI WALIYOIANZISHA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC MAKONDA ATOA SIKU 30 KWA KAMPUNI YA NYANZA KUMALIZA MIRADI WALIYOIANZISHA

Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamiiMKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Mkonda ametoa mwezi mmoja sambamba  na kutopewa kazi nyingine kwa  Kampuni ya Nyanza hadi pale watakapomaliza miradi walioianza.Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati akikagua miradi ya ujenzi wa barabara za halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Amesema barabara hiyo yenye urefu wa kilomita moja inatakiwa kukamilika ndani ya miezi 15 lakini hadi sasa ni miezi 11 ujenzi hauridhishi.
"Mkataba uliosainiwa ni wa miezi 15 hadi sasa ni miezi 11 mradi unasuasu na hauridhishi" amesema Makonda
"Nnaagiza kwa halmashauri zote kampuni hii ya Nyanza isipewe kazi yoyote kwenye Mkoa wangu hadi watakapokamilisha miradi mitatu waliyoianza," ameongeza.
Mkurgenzi wa manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi amesema kampuni imekuwa ikifanya kazi kwa kusuasua hivyo wajitathimini kwa kuwa kwenye halmashauri hiyo hawatapa nafasi.
"Nilipofika Temeke niliwaambia kwenye halmashauri yangu ujanjaujanja hakuna hivyo wajitafakari kwa kina kwani nnaweza kuv... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More