RC Makonda baada ya Dar kuongoza matokeo ya Shule za Msingi ‘asanteni kwa kunivisha nguo na kumpa heshima Rais’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC Makonda baada ya Dar kuongoza matokeo ya Shule za Msingi ‘asanteni kwa kunivisha nguo na kumpa heshima Rais’

Kufuatia Mkoa wa Dar Es Salaam kuongoza katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa Shule za Msingi, RC Paul Makonda ametoa pongezi kwa Walimu, Waratibu Kata, Maafisa Elimu ,Wazazi pamoja na wanafunzi.


Image result for RC Makonda na WalimuRC Paul Makonda

Makonda ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuahidi kutoa zawadi kama motisha kwa Walimu.


Nawapongeza sana sana Walimu, waratibu kata, maafisa Elimu , wazazi pamoja na wanafuzi Kwa kuunganisha nguvu na hatimae tumeongoza ktk matokeo ya darasa la saba Tanzania.Asanteni sana kwakunivisha nguo na kumpa heshima Rais wetu Mpendwa. Ofisi yangu itaandaa utaratibu wa kutowa zawadi kama motisha na Asante Kwa kazi wanayoifanya walimu pamoja na wanafunzi. Tumeongoza tena kwa mara nyingine tena,“ameandika Makonda.


Dar Es Salaam imeongoza kitaifa katika matokeo hayo kwa mwaka wa pili mfululizo ikifuatiwa na Geita, Arusha na Kilimanjaro .The post RC Makonda baada ya Dar kuongoza matokeo ya Shule za Msingi ‘asanteni kwa kunivisha nguo na kumpa heshima Rais’ a... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More