RC Mtwara avunja uongozi wa Ndanda SC na kuunda kamati, Harmonize ndani - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC Mtwara avunja uongozi wa Ndanda SC na kuunda kamati, Harmonize ndani

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gilasius Byakanwa ameamua kuuweka pembeni uongozi wa Ndanda SC uliopo sasa akidai kuwa uongozi huo umeshindwa kuiendesha timu hiyo kiasi cha kuishia kuwa “ombaomba” kila msimu.


Byakanwa ambaye amechukua hatua hiyo akiwa kama mlezi wa timu, ameamua kuunda kamati maalum ya watu 10 itakayosimamia timu hiyo kwa kipindi cha msimu wa ligi kilichosalia.


Mkuu huyo wa mkoa pia amesema atamuomba msanii Harmonize kuwa sehemu ya kamati hiyo endapo ataridhia.


Wanaounda kamati hiyo ni Laurant Paul Werema ambaye atakuwa Mwenyekiti, Stanley Milanzi, Athuman Kambi, Raymond Kasuga, Joseph Peneza, Badwin Masawe, Mohamed Remtulah, Mohamed Nassor, Potensi Rwiza na Said Ally.


“Kuendesha timu kunahitaji pesa, kwahiyo huwezi kuwa na viongozi ambao wakikutana hawawezi hata kununua maji kwaajili ya wachezaji,” amesema Byakanwa.


The post RC Mtwara avunja uongozi wa Ndanda SC na kuunda kamati, Harmonize ndani appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More