RC NDIKILO AKABIDHIWA MIFUKO YA SARUJI 960 KWA AJILI YA KUKARABATI UWANJA WA CCM PICHANDEGE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC NDIKILO AKABIDHIWA MIFUKO YA SARUJI 960 KWA AJILI YA KUKARABATI UWANJA WA CCM PICHANDEGE

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amekabidhiwa mifuko ya saruji 960 kutoka kwa wadau wa maendeleo , kwa ajili ya ukarabati wa uwanja wa Chama Cha Mapinduzi (Sabasaba), Picha Ndege Kibaha ,ambao haujawahi kutumika tangu mwaka 1989.
Uwanja huo unatarajiwa kutumika kwenye maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika viwanda mkoani hapo kuanzia octoba 29-Novemba 4 mwaka huu.Ndikilo alikabidhiwa saruji hiyo kutoka kampuni ya Mwanza Huduma Ltd ambao wametoa mifuko 660 na kampuni ya saruji Kisarawe Lucky Cement Company mifuko 300.
Aidha Ndikilo alielezea ,wameamua kuandaa maonyesho hayo ili kuvitangaza viwanda hivyo na bidhaa wanazozalisha ambapo mkoa unakadiriwa kuwa na viwanda 400."Misaada hii kwani itasaidia kufanikisha ukarabati wa uwanja wa maonyesho hayo yatakayoanza mwishoni mwa mwezi huu," alisema Ndikilo.
Alisema ,maonyesho hayo pia yatahamasisha uwekezaji wa viwanda kwenye mkoa na kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano."Tunaunga mk... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More