RC PWANI AWAONYA WANAOWANYANYASA WAFANYAKAZI WAO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC PWANI AWAONYA WANAOWANYANYASA WAFANYAKAZI WAO

NA VICTOR MASANGU, PWANIWAWEKEZAJI wa sekta ya viwanda wametakiwa kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote za kazi na kuachana na vitendo vya kuvunja sheria za nchi kwa kuamua kuwanyanyasa wafanyakazi wao kwa kuwanyima haki zao za msingi ikiwemo kuwapatia huduma ya matibabu, pamoja na kuwapatia maslahi yao kama inavyotakiwa bila ya kuwa na vitisho vyovyote ili kutumiza azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya uwekeji wa jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengenezea vifungashio (WANDE PRINTING) vitumikavyo katika sekta ya chakula,kilimo,viwanda, afya, ujenzi pamoja na viwanda ambacho kinajengwa katika eneo la kata ya Pangani Wilayani Kibaha na kuwaasa watendaji na mamlaka zinazohusika kuwapa ushirikiano wa kutosha wawekezaji hao bila ya ubaguzi na ubinafsi wowote.
Ndikilo alisema kwamba serikali ya awamu ya tano lengo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More