RC SINGIDA DKT. REHEMA NCHIMBI AWAASA MADAKTARI KUTENDA HAKI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC SINGIDA DKT. REHEMA NCHIMBI AWAASA MADAKTARI KUTENDA HAKI


NA K-VIS BLOG/Khalfan SaidMKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka Madaktari wanaopatiwa mafunzo ya jinsi ya kufanya tathmini kwa mfanyakazi aliyeumia au kuugua mahala pa kazi, kutenda kazi kwa weledi na kwa haraka ili kuharakisha utoaji wa fidia.
Mkuu wa Mkoa alitoa rai hiyo leo Septemba 24, 2018 wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa madakatari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Singida, Dodoma, Kigoma na Tabora kwenye chuo cha Uhasibu Singida.
“Katika kutoa fidia kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi hakuna njoo kesho….njoo kesho, bali ni kumhudumia Mfanyakazi huyo kwa haraka ili aweze kupata fidia yake kutokana na madhara aliyoyapata kwa wakati na ninyi madaktari ndio wenye jukumu kubwa la kuhakikisha mnafanya kazi kwa weledi na kwa haraka.” Alisema.
Dkt. Nchimbi alisema, katika suala la utoaji fidia, Madaktari ni sawa na mahakimu, na wanayo dhamana kubwa sana kwani mapendekezo yao ndiyo yatatoa muongozo kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, kuamua ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More