RC TABORA AAGIZA POLISI KUFANYA DORIA MAENEO YA SHULE ZA MSINGI ILI KUDHIBITI UOVU DHIDI YA WATOTO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC TABORA AAGIZA POLISI KUFANYA DORIA MAENEO YA SHULE ZA MSINGI ILI KUDHIBITI UOVU DHIDI YA WATOTO

NA TTGANYA VINCENT,RS TABORA
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeamua kuweka ulinzi katika shule za Msingi za Manispaa ya Tabora nyakati za masomo ili kuzuia kusije kukatolekea kwa vitendo vyovyote vya kuwazulu na kuwateka wawapo shuleni.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kufuatia vurugu kubwa zilizotokea leo katika Shule ya Msingi Chemuchemu baada ya kuwepo kwa hisia ya watoto wawili kutekwa.
Alisema hadi hivi sasa hajajulikana kama kweli kuna watoto wa Shule hiyo waliotekwa na kupandishwa katika gari aina ya Noah.Mwanri alisema wamejaribu kufuatilia ili kujua ni watoto gani na majina yao ya watoto waliotekwa hakuyapata na wala hakuna mzazi aliyejitokeza kusema kuwa mtoto wake amepotea.
Alitoa wito kama kuna wazazi ambapo watoto wao wametekwa watoe taarifa kwa Polisi au katika Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili hatua ziweze kuchukuliwa ikiwemo kuwatafuta.“Kuanzia sasa nimeagiza Polisi kuongeza Doria katika maeneo y... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More