RC Wangabo afika kwenye ghala la TFC na kukuta patupu - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC Wangabo afika kwenye ghala la TFC na kukuta patupu

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametembela ghala la kuhifadhia mbolea la Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company – TFC) na kutokuta hata mfuko mmoja wa mbolea huku wakulima wakijiandaa na msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 huku mvua zikitarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mh. Wangabo amefanya ziara fupi katika maghala kadhaa ya wafanyabiashara binafsi pamoja na makampuni yaliyopo mjini sumbawanga na kukuta shughuli za uletaji wa mbolea ukiendelea kwa maandalizi yam simu wa kilimo huku Kampuni ya Mboleaa Tanzania (TFC) ikikosa hata mfuko mmoja katika ghala lao jambo lililowashanga walioambatana na Mkuu wa Mkoa katika ziara hiyo.
“Tutawasiliana na viongozi wa TFC ili tuweze kujua kwanini hawaleti mbolea ya kutosha wakati hii ni kampuni ya serikali inaweza ikaleta mbolea nyingi kuliko hata hao wengine lakini badala yake “godown” (ghala) kubwa lakini hakuna kitu, nini manufaa ya TFC sasa,” Alihoji.
Awali akisoma taarifa ya kampuni hiyo msimamizi wa ghala hilo Jel... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More