RC Wangabo aonya vitendo vya Rushwa baraza la Ardhi Sumbawanga - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC Wangabo aonya vitendo vya Rushwa baraza la Ardhi Sumbawanga

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametahadharisha vitendo vya kuchelewesha kusikiliza  mashauri mbalimbali katika baraza la ardhi na nyumba la Wilaya ya sumbawanga hali inayowapelekea wananchi kuhisi kuhusisha ucheleweshaji huo na vitendo vya rushwa na hivyo kuwataka kushikamana na kutafakari kauli mbiu ya wiki ya sheria yam waka huu iliyowataka kutoa haki kwa wakati kwa kushirikiana na wadau.
Amesema kuwa pamoja na mkoa kuwa na baraza moja la wilaya kati ya wilaya zake tatu na hivyo kupelekea kuelemewa na mashauri yanayotoka katika wilaya nyingine za mkoa hiyo isiwe sababu ya wajumbe wa baraza hilo kuchelewesha mashauri jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu.
“Najua kuna mzigo mkubwa na mlundikano wa kesi katika baraza, naambiwa kuna mashauri 399 na mengine 36 yamekaa zaidi ya miaka miwili, lakini pamoja na hayo wananchi nao wanlalamika kuhusiana na baraza la ardhi na nyumba Sumbawanga, moja ya malalamiko makubwa ni kwamba mashauri yanachelewesha amba... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More