RC Wangabo asisitiza upandaji miti kuzuia maafa huku wa mabondeni wakiamuliwa kuhama - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC Wangabo asisitiza upandaji miti kuzuia maafa huku wa mabondeni wakiamuliwa kuhama

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Joachim Wangabo amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri kuhakikisha wanatekeleza sheria ya upandaji miti kwa kila nyumba ili iwe ngao dhidi ya upepo mkali unaosababisha maafa na kuwafanya wanachi hao kukosa mahala salama pa kukaa na wengine kuharibikiwa na vyombo vyao.
Ameyasema hayo alipokwenda kuwatembelea walioathiriwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyoezua paa za nyumba zipatazo 27 na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 26 katika Tarafa ya kirando, Wilayani Nkasi.
“DC tuwe wakali katika hili, kuhakikisha kwamba nyumba ambayo haina miti inayozunguka lile eneo la makazi tuhakikishe kwamba tunachukua hatua stahiki za mazingira, halmashauri mnajua hata kwenye vibali vya ujenzi huwa mnasema lazima muwe na miti angalau minne kama sio mitano lakini hakuna anaefuatilia kwamba hiyo miti ipo? Sadsa ni wakati muafaka wa kufuatilia taratibu zote,” alisisitiza.
Wangabo aliongeza kuwa wale wote waliojenga kwenye mabonde ya mpunga wajue kwamba ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More