RC Wangabo atoa maamuzi mazito baada ya makusanyo ya bilioni 1.34 kuwa mikononi mwa watendaji - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC Wangabo atoa maamuzi mazito baada ya makusanyo ya bilioni 1.34 kuwa mikononi mwa watendajiMkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo

……………………………………………………

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa siku saba kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, kuhakikisha anaunda timu ya uchunguzi ili kuwabaini wadaiwa wa shilingi bilioni 1.34 za makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri na kuwachukulia hatua wahusika wote ili kuleta ustawi katika utekelezaji wa majukumu ya kiserikali.

Amesema hayo baada ya kupitia taarifa za makusanyo na kubaini tatizo la kutowasilishwa kwa makusanyo ya mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa Local Governent Revenue Collection Information System (LGRCIS) na kueleza kuwa kumekuwa na watendaji ambao sio waaminifu wanaokabidhiwa makusanyo hayo na kuyaingiza kwenye matumizi binafsi wakitegemea kurudisha na matokeo yake Bili za wakusanyaji hazikubali kutoka kwenye mfumo hadi fedha zote alizokusanya zitimie.

Akitolea mfano halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mh. Wangabo alisema kuwa “hadi kufikia mwezi Februa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More