RC Wangabo awatahadharisha Wakurugenzi na Madiwani kuhusu mapato - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RC Wangabo awatahadharisha Wakurugenzi na Madiwani kuhusu mapato

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewatahadharisha wakurugenzi wa halmashauri pamojana waheshimiwa madiwani juu ya kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ili kuweza kufikia malengo zaidi ya waliyowekewa na Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Wizara ya OR – TAMISEMI imesema kuwa itawapima wakurugenzi kulingana na makunsanyo ya mapato yao na kuwataka hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha 2018/2019, halmashauri zimetakiwa kufikia asilimia 81 ya ukusanyaji wa mapato.
Katika kuhakikisha azma hiyo inafikiwa Mh. Wanagbo amewaomba waheshimiwa madiwani kuhakikisha kila vikao vyao vinapofanyika agenda ya mapato ipewe kipaumbele na kuwang’ang’ania wakurugenzi na kuwawajibisha wale wote wanaohusika na ukusanyaji wa mapato kwani wao ndio chanzo cha kupata sifa mbaya.
“Waswahili wanasema ‘mchelea mwana kulia hulia yeye’ sasa kama tutawalealea hawa ambao wanatusababishia sisi tusikusanye mapato matokeo yake mkichelea kwenu nyinyi kama viongozi na wawakilishi w... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More