REFA MJERUMANI AMLIMA KADI YA NJANO SAMATTA GENK IKILAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA AKINA PEPE ULAYA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

REFA MJERUMANI AMLIMA KADI YA NJANO SAMATTA GENK IKILAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA AKINA PEPE ULAYA

Na Mwandishi Wetu, GENK
REFA Mjerumani, Tobias Stieler jana amemuonyesha kadi ya njano mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta timu yake, KRC Genk ikilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Besiktas ya Uturuki katika mchezo wa Kundi I UEFA Europa League.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, Samatta alikuwa na wakati mgumu mbele ya mabeki wa Besiktas walioongozwa na mkongwe, beki wa zamani wa Real Madrid, Kleper Laveran Lima Ferreira maarufu Pepe na kisiki cha Croatia, Domagoj Vida na haikuwa ajabu alipoonyeshwa kadi ya njano dakika ya 35. 
Nahodha wa Tanzania, Samatta naye akamsababishia kadi ya njano pia, beki wa Ureno Pepe dakika ya 80, wakati mchezaji mwingine aliyeonyeshwa kadi ya njano jana ni Necip Uysal dakika ya 15.
Refa Mjerumani, Tobias Stieler (kulia) akimuonyesha kadi ya njano mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta jana 


Mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta akijitetea mbele ya refa Tobias Stieler kabla ya kuonyeshwa kadi ya njano... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More