REFA WA NAMIBIA ‘AWACHOMA’ RWANDA WALITAKA KUMPA RUSHWA AWABEBE MECHI NA IVORY COAST - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

REFA WA NAMIBIA ‘AWACHOMA’ RWANDA WALITAKA KUMPA RUSHWA AWABEBE MECHI NA IVORY COAST

Na Mwandishi Wetu, KIGALI
VIONGOZI wawili wa soka wa Rwanda wamewekwa rumande kwa tuhuma za kutaka kumhonga refa Jackson Pavaza wa Namibia aisaidie timu ya taifa ya nchi hiyo, Amavubi kushinda dhidi ya Ivory Coast.
Shirika la Uchunguzi la Rwanda (RIB) Alhamisi jana lilisema kwamba lilikuwa linawashikilia viongozi wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo (FERWAFA), Katibu Mkuu Francois Regis Uwayezu na Kamishna wa Mashindano Eric Ruhamiriza kwa tuhuma hizo.
Wanadaiwa kutaka kumhonga fedha refa Pavaza aisaidie Amavubi kushinda dhidi ya Tembo wa Ivory Coast mechi ya Kundi H kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika iliyofanyika Jumapili iliyopita Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.

Refa wa Jackson Pavaza (katikati) akiwaongoza wachezaji wa Rwanda na Ivory Coast kuingia uwanjani Jumapili mjini Kigali

Ivory Coast ilishinda 2-1, mabao yake yakifungwa na Jonathan Kodjia dakika ya 45 na Max-Alain Gradel dakika ya 49, wakati la Rwanda lilifungwa na mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere daki... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More