Rekodi hazidanganyi aisee, Mbappe ni zaidi ya Cr7 na Lionel Messi - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rekodi hazidanganyi aisee, Mbappe ni zaidi ya Cr7 na Lionel Messi

Achilia mbali kama ndiye mchezaji bora chipukizi wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 lakini akiwa na umri chini ya miaka 20 tayari Kylian Mbappe ameshabeba kombe hilo.


Mbappe amebeba kombe ambalo watawala wawili wa soka kwa takribani miaka 9 sasa Cristiano Ronaldo na mwenzake Lionel Messi hawajawahi kulibeba.Takwimu zinaonesha pamoja na Messi na Ronaldo kuwa wafalme wa soka la ulimwengu huu lakini kati ya hao wawili hakuna aliyemzidi Mbappe wakiwa na umri kama alionao kwa sasa.


Akiwa na miaka 19 tu Kylian amwshafunga jumla ya mabao 52 katika misimu miwili ambayo amekuwa akicheza katika ligi kuu nchi Ufaransa Ligue 1.Mabao 52 ni idadi ambayo sio Messi wala Cr7 ambaye amewahi kuyafunga katika umri huu kwani Cristiano Ronaldo yeye katika umri kama wa Mbappe alifunga mara 17.


Nyota wa timu ya taifa ya Argentina pamoja na klabu ya Barcelona Lionel Messi yeye akiwa na umri kama wa Kylian Mbape alifunga mabao 25 tu.Sii hivyo tu kwani katika Champions League Kylian Mbape ameshaziti... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More