Rich Mavoko aliza watu mtandaoni kwa ujumbe mzito, adai mwisho wa maisha yake umefika - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rich Mavoko aliza watu mtandaoni kwa ujumbe mzito, adai mwisho wa maisha yake umefika

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rich Mavoko ameacha ujumbe mzito kwenye mitandao ya kijamii ulizua gumzo usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2019.

Rich Mavoko

Rich Mavoko kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kwa ufupi, akidai kuwa leo ndio mwisho wa maisha yake hapa duniani.

Ni Siku Ya Mwisho Ya Maisha Yangu Yaliobaki” ameandika Rich Mavoko na kuambatanisha picha akiwa mwenye pozi la huruma.

Baadhi ya posti hiyo, wadau mbali walianza kuhoji ni nini? kimejili au kumkuta hadi aweke ujumbe huo huku wengine wakimdhihaki.

teresiamassawe-Wewe mavoko ni kiki unatafuta siyo? Nakuliza?Usimbipu mungu atakupigia.We kama unataka kuachia ngoma mpya lazima urushe vitu vya ajabu mtandaoni? Tena kibaya zaidi eti unasema kifo? Kama ni uwongo utakiona cha moto we haya.selemanzubery28-duh!!!!! unaniliza bro sana maana na kukubali ile mbaya mwanangu please please usifanye hivyoluchax_tz-Kunani tena ama ni ile hatrick ya ronaldo ndo inakupa stress c’mon bongo flavor’s Messi... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More