Rich Mavoko awashukuru BASATA kwa kupokea malalamiko yake na WCB ‘hata iweje nyie ndio walezi wa sanaa yetu’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rich Mavoko awashukuru BASATA kwa kupokea malalamiko yake na WCB ‘hata iweje nyie ndio walezi wa sanaa yetu’

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Rich Mavoko amejitokeza kwa mara ya kwanza kuelezea sakata la kukutana na BASATA kuwasilisha mkataba wake aliosaini na WCB aliodai kuwa unamkandamiza.


Rich Mavoko

Mavoko kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa anashukuru kukutana na BASATA na kupata elimu ya kutosha huku akiwamwagia sifa kuwa hao ndio maana halisi ya walezi wa sanaa yetu nchini Tanzania.Nimejifunza vingi ila la muhim  kabisa  nimeona Umuhim wa kukaa karibu na  walezi wetu mana changamoto ni nyingi na  kuna mengi ila yote mnaweza yajua kama tukiwa karibu nanyi leo mmenipa maana ya neno mama ni mama ata kama ni kilema, ata iweje nyinyi ndo walezi wasanaa Yetu Niseme Tu Asante #Basata


A post shared by Billionaire kid£££ (@richmavoko) on Aug 9, 2018 at 10:16am PDT

Leo Alhamisi Agosti 9, 2018 Rich Mavoko amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza ambapo amepeleka mkataba wake na WCB akidai uangaliwe upya kwani umekuwa ni wa unyonyaji.


The post Rich ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More