RIDHIWANI KIKWETE ATOA MISAADA KATA YA UBENA ZOMOZI HUKO CHALINZE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RIDHIWANI KIKWETE ATOA MISAADA KATA YA UBENA ZOMOZI HUKO CHALINZE

NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE 
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya saruji 20 na matofali 3,000 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi wa shule ya msingi katika kitongoji cha Choza .
Aidha amemkabidhi msaada wa baiskeli ya miguu mitatu (wheel Chair),mkazi wa Zomozi-Ubena mzee Cosmas Alphonce Chongwe ambae ni mlemavu wa miguu.
Katika hatua nyingine ,Ridhiwani alitoa fimbo nne maalum kwa ajili ya walemavu wa macho,kadi 23 za afya kwa ajili ya matibabu ya wazee, vyote vikiwa na thamani zaidi ya sh.milioni tano.
Mbunge huyo alitoa misaada hiyo baada ya kumaliza kikao chake alichofanya pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Ubena-Zomozi.
Ridhiwani alieleza, msaada huo alioutoa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Ilani ya uchaguzi na maombi mbalimbali ya wananchi katika kata hiyo. 
Pamoja na hayo, alikutana na wanachama mbalimbali wa vikundi vya maendeleo katika kata hiyo, ambapo aliwahimiza kuendelea kujiung... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More