Ripoti nyeti ya Stiegler’s Gorge yazinduliwa, Yapangua hoja potofu za UNESCO, WWF kuhusu uamuzi wa Rais Dk. Magufuli - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ripoti nyeti ya Stiegler’s Gorge yazinduliwa, Yapangua hoja potofu za UNESCO, WWF kuhusu uamuzi wa Rais Dk. Magufuli


TIMU ya wataalamu bingwa watano wa Kitanzania waliobobea katika masuala ya uhifadhi, mazingira na uchumi, juzi ilizindua ripoti yake ya utafiti wa kitalaamu kuhusu faida na madhara ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kufua umeme wa Mto Rufiji, unaofahamika zaidi kama Stiegler’s Gorge Hydropower Project.

Ripoti hiyo imezinduliwa zikiwa zimesalia takriban siku saba kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa na Kampuni inayomilikiwa na Serikali ya Misri,inayofahamika kwa jina la Arab Contractors.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Hotel ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam, kiongozi wa timu hiyo wa wataalamu, Saleh Pamba alisema utafiti wao ulilenga kuangalia madhara na faida za ujenzi wa mradi baada ya mashirika mawili ya umoja wa mataifa kujitokeza hadharani kupinga azma ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, kuutekeleza.

Pamoja na Pamba, wataalamu wengine katika timu hiyo ni Dk. Abubakar Rajab, Abdulkarim Shah, Dk. Magnus Ngoile na Dk. Thomas... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More