Riyama Ally Akimbilia Kwenye Muziki. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Riyama Ally Akimbilia Kwenye Muziki.

Msanii wa maigizo na vichekesho nchini , Riyama Ally amefunguka jinsi alivyofurahi kupewa heshima na wasanii wa kundi la ROSTAM kwa kuingiza kionjo katika wimbo huo ambacho kimefanya wimbo kunoga zaidi.


Mwanadada huyo anasema kuwa kwake ni heshima kubwa lakini pia amefurahi kuona wimbo umepokelewa vizuri hata kama sio wa kwake lakini ameweka mkono wake pale na imekuwa ikifanya vizuri.


akiongea katika kipindi cha papaso la burudani Riama anahadithia ilivyokuwa kabla ya wimbo kutoka ‘meneja wa ROSTAm alinipigia simu akaniambia kuwa kuna sauti inatakiwa kuigizwa kwenye wimbo na mimi ndio mhusika, nikafika studio nikaingiza kile kionjo chini ya usimamizi wa mume wangu  nashukuru sana kwa sababu wimbo umetoka na umependwa


Mwanadada huyo anaeonekna kuwa na Vipaji vingi amekuwa moja ya chachu za sanaa kwa kazi zake nzuri anazofanya zinazoendana na uhalisia.


The post Riyama Ally Akimbilia Kwenye Muziki. appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More