#RoadToRussia, kina Messi na Dyabala wapewa somo namna ya kuwapata wanawake wa Kirusi - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

#RoadToRussia, kina Messi na Dyabala wapewa somo namna ya kuwapata wanawake wa Kirusi

Hakuna kipindi ambacho kuna habari nyingi za kushangaza na kustaajabisha kuhusu michuano ya kombe la dunia kama kipindi hiki, kila siku kunaibuka hili na hii yote inaonesha michuano hii imeshafika.


Katika hali ambayo sio ya kawaida, chama cha soka nchini Argentina kimejikuta katika vichwa vya habari duniani baada ya kutoa maelekezo ya jinsi ya kutongoza wanawake wa Kirusia kwa timu yao inayokwenda Urusi.


Katika maelekezo ambayo haswa yalikuwa na nia ya jinsi ya kuwafundisha Argentina namna ya kuishi wakiwa Urusi na lugha inayotumiwa huko kwa ujumla, lakini kulikuwa na kipengele pia cha kuhusu wanawake.


Katika waraka huo ambao hutolewa kwa wachezaji na waandishi watakaosafiri na timu inaelekeza namna ambavyo unatakiwa kumfanya mwanamke wa Kirusi kujisikia fahari wakati wa michuano hiyo.


Lakini baada ya maelekezo hayo kuvuja, raisi wa chama cha soka Argentina Claudio Tapia ameomba msamaha kwa tukio hilo na kusisitiza kwamba chapisho hilo lilikuwepo bahati mbaya na hawajui nani ameliweka.... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More