#RoadToRussia, unajua kadi nyekundu “umeme” na rekodi zake kombe la dunia? - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

#RoadToRussia, unajua kadi nyekundu “umeme” na rekodi zake kombe la dunia?

Watoto wa mjini wanauita “umeme”, sisi waswahili tunaijua kama kadi nyekundu. Hii ni adhabu ya mwisho kabisa katika soka ambapo ukipewa adhabu hii baasi ni moja kwa moja nje ya uwanja.


Kwa mara ya kwanza kabisa katika michuano ya kombe la dunia kadi nyekundu ya kwanza ilitolewa katika kombe la dunia la mwaka 1930 ambapo mwaka huu michuano ya kombe la dunia ilifanyika nchini Uruguay.


Placido Galindo ambaye ni raia wa Peru alikuwa mchezaji wa kwanza kupewa umeme ambapo hii ilikuwa wakati wa mchezo kati ya Peru ambao walikuwa wakicheza dhidi ya Romania.


Bado hakuna mtu aliyevunja rekodi ya Jose Batista huyu alikuwa Mruguay, Batista anashikilia rekodi ya kadi nyekundu ya mapema zaidi ambapo alipewa kadi hiyo dakika ya kwanza tu ya mchezo katika mechi yao dhidi ya Scotland.


Mwaka 2006 ndio mwaka ambao Zinedine Zidane naye alioneshwa umeme na ni mwaka huu ambao kwa rekodi za kombe la dunia inaonesha kulikuwa na kadi nyingi zaidi za kombe la dunia, zilikuwa 28.


Claudio Cannigia raia wa Ar... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More