Roma awatolea uvivu BASATA ‘mnaua sanaa, ubunifu na vipaji. hivi wimbo wa Parapanda una matatizo gani?’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Roma awatolea uvivu BASATA ‘mnaua sanaa, ubunifu na vipaji. hivi wimbo wa Parapanda una matatizo gani?’

Rapa Roma Mkatoliki ameamua kufunguka na kuweka wazi hisia zake dhidi ya BASATA kwa kudai kuwa wanaua Sanaa, ubunifu na vipaji vya Watanzania.


Roma Mkatoliki

Roma kupitia ukurasa wake wa Twitter amefunguka hayo na kuwaomba Watanzania waeleze makosa yanayopatikana kwenye wimbo wao mpya na Stamina wa Parapanda.


“BASATA You Are Killing 1. An Art 2. Creativity 3.Talent I don’t Hate The Industry I hate The System!! Hivi Wimbo Wa PARAPANDA Una Matatizo Gani??? Hebu Nisaidie Wewe Mtanzania Mwenzangu!!!!”ameeleza Roma Mkatoliki.


Leo Agosti 6, 2018 Roma na Stamina waliitwa BASATA ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa BASATA kwenye mahojiano Yake mafupi na Bongo5 alisema waliwatembelea tu kujua Sheria na kanuni mpya za baraza hilo. 


The post Roma awatolea uvivu BASATA ‘mnaua sanaa, ubunifu na vipaji. hivi wimbo wa Parapanda una matatizo gani?’ appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More