RUDI TTCL KUMENOGA-MWANRI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RUDI TTCL KUMENOGA-MWANRI


NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

WAKAZI wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuliunga mkono Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujiunga na huduma mbalimbali wanazotoa ili liweze kuendelea kutoa gawio kubwa kwa Serikali kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi wote hapa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya rudi nyumbani kumenoga mkoani humo.

Alisema kuwa kupitia gawio ambalo Shirika hilo linatoa kwa Serikali kati ya fedha hizo zinakuja Mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara, huduma za maji, shule , ununuzi wa dawa, ulipaji wa mishahara ya watumishi na shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Ndugu zangu TTCL kumenoga turudi…ukiongeza salio kwenye simu yako hata usipotumia mwezi salio lako liko salama…hivi sasa huduma zao hazihitaji kupanda kwenye mti ndio ufanye mawasiliano, bali popote unawasiliana…hakuna kusema sogea pembeni sikusikii ndio upige simu…hiv... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More