RUTA KUFANYA MAANDAMANO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DK. MAGUFULI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RUTA KUFANYA MAANDAMANO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DK. MAGUFULI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
UMOJA wa wananchi ujulikanao kama Rudisha Uzalendo Tanzania (RUTA) unatarajia kufanya maandamano ya amani ya kumuunga mkono Rais John Magufuli kutokana na juhudi na uthubutu anaoonesha katika utendaji wake wa kazi yatakayofanyika jijini Dar es salaam.
Akizungumza na vyombo vya habari Mwenyekiti wa Kamati ya maandamo hayo Charles Maselle ameeleza kuwa Juni 21, mwaka huu watafanya maandamano ya amani yasiyohusisha itikadi za vyama vya kisiasa wala dini ila wananchi wa kada zote jijini wataandamana kutoka Karume na kumalizikia katika viwanja vya mnazi mmoja na wanategemea mgeni rasmi atakuwa Rais.
Aidha amesema kuwa kama wananchi wameona ni bora kumpongeza Rais kwa sasa ili kumpa nguvu na kumtia moyo katika kazi anazofanya hasa dhamira yake ya dhati, ukweli na uthubutu katika kuleta maendeleo na wameanza kwa mkoa wa Dar es salaam na baadaye yataendelea nchini kote.
Pia Maselle ameeleza kama wananchi wameamua kurudisha uzalendo kutokana na mambo yanayofanywa ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More