RUVU SHOOTING WADAI NYEKUNDU NDIYO ILIYOWAPONZA KUPIGWA NNE NA MBEYA CITY JANA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RUVU SHOOTING WADAI NYEKUNDU NDIYO ILIYOWAPONZA KUPIGWA NNE NA MBEYA CITY JANA

Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Ruvu Shooting jana kilishuka kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kucheza dhidi ya Mbeya City na kufungwa mabao 4-2.
Katika mchezo huo, wachezaji nane wa Ruvu Shooting walizuiliwa na Shirikisho la Soka Tanzania TFF kucheza kutoka na vibali vyao kuchelewa kutoka.
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kikosi cha timu yake kilikua na wachezaji 12 ambapo 11 walianza na mmoja ambaye ni beki alibaki akiwa ni mchezaji wa akiba.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – online, Bwire amesema licha ya kikosi hicho kuwa na wachezaji wachache, dakika za mwanzoni kabisa za mchezo huo mchezaji wao Ayoub Kitala alitolewa na mwamuzi kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga Nchunga Said wa Mbeya City.
Ruvu Shooting jana imechapwa mabao 4-2 na Mbeya City Uwanja wa Sokoine

Alisema kadi hiyo nyekundu iliwatoa mchezoni wachezaji wote kutoka mchezoni na kuruhusu mabao yote manne. “Tumesafiri Mbeya na wachezaji 18 lakini kati yao wachezaji nane TFF ikasema hawana s... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More