RvP aitaja mechi ngumu kabisa kuwahi kucheza maishani - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

RvP aitaja mechi ngumu kabisa kuwahi kucheza maishani

Moja kati ya washambuliaji hatari kuwahi kutokea katika ligi ya Epl ni Robin Van Persie, Van Persie maarufu kama RvP alikuwa nyota chini ya Arsene Wenger na baadae akawika tena chini Louis Van Gaal akiwa Manchester United.


Kwa sasa Robin Van Persie anacheza katika timu ya kwao ya Uholanzi katika klabu ya Feyenoord bado ana kumbukumbu kubwa kuhusu ligi ya Uingereza, Van Persie anaamini mechi ngumu zaidi kwenye maisha yake aliicheza EPL.


Ni Stoke City, Van Persie anaamini tangu aanze soka katika ngazi ya uweledi hajawahi kucheza mchezo mgumu au kwenda safari ngumu kama safari ya kwenda Britannia Stadium kuikabili Stoke City.


Van Persie ameuelezea mchezo wao dhidi ya Stoke City kwamba ilikuwa kama vita kwa namna Stoke walivyokuwa wanacheza, na takwimu zinaonesha kweli RVP alikuwa na kipindi kigumu Britannia kwani katika mechi 6 katika dimba hilo alipoteza 3,suluhu 2 na kushinda1 tu.


Swansea, Bolton na Sheffield United ni timu nyingine ambazo Van Persie hatakuja kuzisahau, na kubwa anasema... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More