Rwanda yapiga marufuku ndege aina ya Boeing 737 Max kuruka katika anga yake, yaungana na mataifa mengine duniani - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Rwanda yapiga marufuku ndege aina ya Boeing 737 Max kuruka katika anga yake, yaungana na mataifa mengine duniani

Shirika la usafiri wa ndege Rwanda limetoa agizo kwa marubani na kampuni za ndege kutoendesha ndege za Boeing 787 Max 8 na Max 9 katika anga ya Rwanda.





Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Rwanda sasa imejiunga na mataifa mengine duniani ambayo yamepiga marufuku usafiri wa ndege hizo za aina ya Boeing 787 Max 8 na Max 9.





Hii inafuata ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines Jumapili ilioanguaka muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu Addis Ababa na kusababisha vifo vya watu 157.





Taarifa zinaeleza kwamba Rwanda ilikuwa na mipango ya kukodisha ndege mbili za aina hiyo Boeing 737- 800.





Hatahivyo, huenda mipango hiyo ikasitishwa kwa muda sasa wakati kukisubiriwa uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoanguka Jumapili nje kidogo ya mji mkuu Addis Ababa.





Ndege kama hiyo ya kampuni ya Lion Air, ilianguka kutoka pwani ya Indonesia Oktoba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 189.





Katika taarifa rasmi iliyowekwa kwenye mtandao wa twitter ya mkurugenzi mkuu ka... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More