SADC KUTENGENEZA AJIRA ZAIDI YA 5000 NA KUINGIZA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 10 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SADC KUTENGENEZA AJIRA ZAIDI YA 5000 NA KUINGIZA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 10

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amewataka wamiliki na wafanyabiashara wa Hoteli Jijini Dar es salaam kutumia fursa ya kibiashara itakayotokana na ujio wa wageni takribani 1000 watakaoshiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuanzia mwezi August 2019.
Waziri Prof Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli na kuongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itafanya kazi kwa ukaribu na wadau hao wa Hoteli na kuwataka kutoa huduma bora,bidi,weledi na kwa uzalendo usiotiliwa mashaka ili waweze kunufaika na uwepo wa ugeni huo mkubwa wa SADC.
“Ninyi ni watu muhimu sana katika ugeni huu wa SADC,tushirikiane kuufanya mkutano huu kuwa wa mafanikio makubwa kwa ukarimu na uzalendo wetu na hivyo kutufanya pia kuingiza kipato katika biashara zetu kwa kuwa tukifanya vizuri kila watakapokuwa wanakuja... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More