Sakata la KKKT Lamfukuzisha Kazi Msajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Sakata la KKKT Lamfukuzisha Kazi Msajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Mwigulu Nchemba amesimamisha kazi Msajili wa Taasisi za Dini Maryline Komba huku akiwaomba viongozi wa dini kuendelea na shughuli zao za kutoa huduma za kiroho.  
Waziri Mwigulu ameyasema hayo wizarani hapo wakati alipotangaza kumsimamisha kazi na  kupisha uchunguzi wa kina na iwapo atabainika kutohusika na matamko hayo au nyaraka ambazo zinasambaa mtandaoni basi atarudi kwenye majukumu yake.  
Wizara yake inaendelea kuchunguza aliyeandika na kusambaza nyaraka katika mitandao ya kijamii ambayo imeibua sintofahamu kwa viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla ili sheria ichukue mkondo wake.  
“Serikali na viongozi wa dini wamekuwa na ushirikiano mkubwa na hakuna mahali ambapo wanaonekana kutoaminiana.Hivyo aliyesambaza nyaraka hizo tunachunguza na kisha tutachukua hatua zinazostahili,”amesema Dk.Mwigulu.  
Amesema viongozi wa dini na watanzania kwa ujumla wafahamu kuwa nyaraka na matamko ambayo yamesambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina b... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More