SAKATA LA KUPOTEA 'MBWA ASKARI'LACHUKUA SURA MPYA, WAZIRI AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE, IGP SIRRO APEWA JUKUMU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAKATA LA KUPOTEA 'MBWA ASKARI'LACHUKUA SURA MPYA, WAZIRI AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE, IGP SIRRO APEWA JUKUMU

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amesma wamekubaliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchin IGP Simon Sirro kuanza uchunguzi wa kina kuhusu mbwa aliyepotea.
Amefafanua mbwa aliyepotea anayo mafunzo yote ya kukamata wahalifu na anao uwezo mkubwa wa kukabiliana na matukio ya kihalifu kama askari,hivyo kupotea kwa mbwa huyo lazima uchunguzi huo ufanyike.
Lugola ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema tayari IGP Sirro amemueleza kuwa ameanza uchunguzi wa mbwa huyo na kwamba ni vema mjadala wa mbwa huyo ukasitishwa ili uchunguzi ufanyike.
Amefafanua katika ziara ambayo ameifanya hizo hivi karibuni katika vyombo vya ulinzi na usalama amepata nafasi ya kwenda katika kikosi cha mbwa na farasi."Mbwa na farasi walioko kwenye kikosi hicho wanatengewa fedha za chakuka na malazi.Mbwa na Farasi hao wanafanya kazi mbalimbali za ulinzi,"amesema Lugola.
Ameongeza maelezo ambayo aliyapata akiwa katika kikosi cha farasi na mbwa ... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More