SALAH AFUNGA DAKIKA YA MWISHO MISRI YAICHAPA TUNISIA 3-2 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SALAH AFUNGA DAKIKA YA MWISHO MISRI YAICHAPA TUNISIA 3-2

MSHAMBULIAJI Mohamed Salah jana amefunga bao la dakika ya mwisho kuisaidia Misri kutoka nyuma na kushinda 3-2 dhidi ya Tunisia katika mchezo wa Kundi J Kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
Morocco iliifunga Cameroon 2-0 mjini Casablanca na sasa wanahitaji pointi moja kujihakikishia nafasi ya kwenda fainali za mwakani, wakati Burundi imekaribia kufuzu kwa mara ya kwanza baada ya ushindi wa 5-2 ugenini dhidi ya Sudan Kusini.
Misri na Tunisia tayari zimefuzu kutoka Kundi J, lakini mchezo baina yao ulikuwa una upinzani mkali hususan baada ya Esperance ya Tunisia kuinyuka Al Ahly ya Misri na kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Naim Sliti alianza kuifungia Tunisia dakika ya 13 kabla ya Misri kusawazisha kupitia kwa Mahmoud 'Trezeguet' Hassan.
Baher El Mohamady akaifungia Misri bao la pili dakika ya 59, lakini beki mwenzake Ahmed Hegazi akampa nafasi Sliti kuifungia tena Tunisia zikiwa zimesalia dakika tano kabla ya Salah kufunga la ushindi dak... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More