SALAH MWANASOKA BORA AFRIKA, DENIS ONYANGO AWA KIPA BORA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SALAH MWANASOKA BORA AFRIKA, DENIS ONYANGO AWA KIPA BORA

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2018 kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya miezi 12 mizuri.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Misri ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwasaidia Wekundu hao kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei mwaka jana na amekuwa chachu ya mafanikio ya Liverpool kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England hadi sasa ikiwa inaongoza. 
Katika sherehe zilizofanyika mjini Dakar, Senegal, usiku wa jana, Salah ametetea tuzo aliyoitwaa miezi 12 iliyopita.
Salah aliweka rekodi ya mabao msimu wa 2017/18 kwa kufunga mabao 32 kwenye Ligi Kuu nya England na 44 jumla katika mashindano yote.


Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia, George Weah akimkabidhi Mohamed Salah tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika jana mjini Dakar, Senegal PICHA ZAIDI GONGA HAPA Pia alifunga mabao mawili katika fainali za Kombe la Dunia mwaka jana ambazo zilikuwa za kwanza kwa Misri baada ya miaka 28.
Salah amemshinda mchezaji mwenzake wa Liverpool, Sadio Mane na nyota wa... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More