SALAMBA AKOSA PENALTI SIMBA SC YALAZIMISHA SARE 1-1 NA ASANTE KOTOKO UWANJA WA TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SALAMBA AKOSA PENALTI SIMBA SC YALAZIMISHA SARE 1-1 NA ASANTE KOTOKO UWANJA WA TAIFA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Asante Kotoko ya Ghana katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam jioni leo.
Ulikuwa mchezo mzuri uliotanguliwa na shamrashamra za tamasha la Simba Day kwa burudani mbalimbali zikiwemo za muziki kutoka kwa wasanii tofauti, ambalo lilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kama mgeni rasmi.  
Simba SC walio chini ya kocha Mbelgiji, Patrick J Aussems waliuanza vizuri mchezo huo wakisukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Kotoko, lakini safu ya ulinzi ya timu ya Ghana ilikuwa imara mno.
Washambuliaji wa Simba, Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere na Mganda Emmanuel Okwi walicheza kwa uelewano mkubwa na kutengenezeana nafasi kadhaa, lakini kipa wa Kotoko, Felix Annan aliokoa kwa ustadi mkubwa.
Adam Salamba (kulia) akisikitika baada ya kukosa penalti leo 
Emmanuel Okwi (kushoto) akifumua shuti katika mchezo wa leo
Cletus Chama akitoa pasi baada ya kuwato... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More