SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

Uongozi na watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ( Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) tunaungana na ndugu, jamaa na Watanzania wote katika kuombeleza msiba mzito kwa Taifa baada ya ndugu zetu wapendwa kupoteza maisha katika ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea katika Ziwa Victoria, tarehe 20 Septemba, 2018.
Tunatoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli , ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto22/09/2018... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More