SAM MANGWANA ASIYEKATA TAMAA KATIKA MUZIKI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAM MANGWANA ASIYEKATA TAMAA KATIKA MUZIKI

Na: Moshy Kiyungi, Dar es Salaam
Machi, 2019.
Majina ya Sam Mangwana siyo mageni masikioni mwa wapenzi wa muziki wa dansi Afrika Mashariki na Kati. Ni mwanamuziki mwenye vipaji vya utuzi na kuimba nyimbo za muziki wa dansi.
Wasifu wa Sam Mangwana unaeleza kuwa alizaliwa Februari 21, 1945, katika mji wa Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wazazi wake walikuwa wahamiaji ambapo baba yake alikuwa raia toka nchini Zimbabwe, wakati mama yake raia wa  Angola. Mangwana aliwahi kuwa mwanachama, mtunzi na mwimbaji katika bendi ya T.P. OK Jazz, iliyokuwa ikiongozwa na Franço Luambo Makiadi.
Nguli huyu alipitia kupiga muziki katika bendi zilizokuwa zikiongozwa na Tabu Ley Rochereau za African Fiesta, African Fiesta National na Afrisa Internationale.
Weledi wake katika muziki ulijulikana zaidi mwaka 1963, alipokuwa akipiga muziki wa rhumba katika bendi ya African Fiesta, iliyokuwa ikimilikiwa na na kuongozwa na Tabu Ley Rochereau.
Baadae Sam Mangwana alivuka mto Kongo akaingia katika mji wa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More