SAMATTA AFUNGA NA KUSABABISHA BAO KRC GENK IKIICHAPA CLUB BRUGGE 3-1 LIGI YA UBELGIJI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAMATTA AFUNGA NA KUSABABISHA BAO KRC GENK IKIICHAPA CLUB BRUGGE 3-1 LIGI YA UBELGIJI

Na Mwandishi Wetu, GENK
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku huu amesababisha bao la pili na kufunga la tatu kuisaidia timu yake, KRC Genk kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Club Brugge katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Leandro Trossard alifunga bao la kwanza dakika ya 13, kabla ya H. Vanaken kuisawazishia Club Brugge kwa penalti dakika ya 36.
Mbwana Samatta akapiga shuti likambabatiza beki wa Club Brugge na Ruslan Malinovskiy akaenda kufunga kwa penalti dakika ya 55.

Mbwana Samatta amefunga na kusababisha bao KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Club Brugge 

Ukawadia wakati wa Mbwana kufunga mwenyewe dakika ya 81 , hilo likiwa bao lake la 21 msimu huu na kuihakikishia Genk ushindi wa tatu katika mechi nne za hatua ya pili ya Ligi ya Daraja la Kwanza A Ubelgiji, maarufu kama Championship Round.
Samatta mwenye umri wa miaka 26, usiku huu amecheza mechi ya 150 kwenye mashindano yote na akiwa amefunga mabao... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More