SAMATTA AISAIDIA GENK KUTWAA TAJI LA SUPER CUP YA UBELGIJI, YAIPIGA MECHELEN 3-0 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAMATTA AISAIDIA GENK KUTWAA TAJI LA SUPER CUP YA UBELGIJI, YAIPIGA MECHELEN 3-0

Na Mwandishi Wetu, GENK 
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta  jana ameisaidia klabu yake, KRC Genk kutwaa Super Cup ya Ubelgiji baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KV Mechelen Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Huo ulikuwa ni mchezo wa kuunganisha mataji baina ya mabingwa wa Ligi, KRC Genk dhidi ya washindi wa Kombe KV Mechelen kuashiria ufunguzi wa msimu mpya nchini humo.
Na mabao ya Genk yalifungwa na beki mwenye umri wa miaka 28, Sebastien Dewaest dakika ya 14 na 60 na mshambuliaji kinda wa umri wa miaka 21, Dante Vanzeir la tatu dakika ya 83, wote Wabelgiji.
Mbwana Samatta akifurahia na taji la Super Cup ya Ubelgiji baada ya kuiwezesha Genk kushinda 3-0 dhidi ya KV Mechelen  
Mbwana Samatta akifurahia wenzake taji la Super Cup ya Ubelgiji baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya KV Mechelen  
Mbwana Samatta akiondoka na mpira katikati ya wachezaji wa KV Mechelen 

Samatta alicheza kwa dakika 71 tu mchezo huo wa kwanza kwake wa msimu kabla ya kumpisha Vanzeir aliye... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More