SAMATTA AKOSA BAO LA WAZI DAKIKA ZA MWISHONI KRC GENK YACHAPWA 3-2 UGENINI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAMATTA AKOSA BAO LA WAZI DAKIKA ZA MWISHONI KRC GENK YACHAPWA 3-2 UGENINI

Na Mwandishi Wetu, BRUGGE
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amekosa bao la wazi dakika za mwishoni, timu yake KRC Genk ikichapwa 3-2 na wenyeji, Club Brugge katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Jan Breydel mjini Brugge.
Samatta aliunganishwa kwa kichwa krosi kutoka kushoto, mpira ukagonga mwamba na kumrudia akajaribu kupiga tena, lakini beki mmoja wa Club Brugge akaunawa katika harakati za kuokoa, ingawa refa Bram Van Driessche ‘akakausha’.
Wakati Genk ilikuwa tayari nyuma kwa 3-2, mabao ya Club Brugge yakifungwa na Hans Vanaken dakika ya 53, Lois Openda dakika ya 63 na Krepin Diatta dakika ya 68 wakati ya wageni yalifungwa na Sebastien Dewaest dakika ya nne na Zinho Gano dakika ya 88.
Mbwana Samatta akisikitika baada ya kukosa bao la wazi wakati huo huo refa akiwanyima penalti

Pamoja na kufungwa, Genk bado inagongoza kwa pointi zake 50 ikifuatiwa na Club Brugge yenye pointi 47 sasa. Genk ilihitaji ushindi leo ili kutangaza ubingwa na sasa... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More