SAMATTA ALIMWA KADI YA NJANO KRC GENK YAWABABUA ANDERLECHT 1-0 LIGI YA UBELGIJI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAMATTA ALIMWA KADI YA NJANO KRC GENK YAWABABUA ANDERLECHT 1-0 LIGI YA UBELGIJI

Na Mwandishi Wetu, GENK
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana usiku ameonyeshwa kadi ya njano timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 1-0 RSC Anderlecht katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, Samatta alionyeshwa kadi ya njano dakika ya mwisho kabisa, ya tano ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo. 
Na hiyo ilikuwa kadi ya nane ya njano jumla anaonyeshwa katika muda wote wa kuichezea Genk tangu amejiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na bahati nzuri kwake hajawahi kuonyeshwa kadi nyekundu kihistoria.
Mbwana Samatta akipambana katika mechi ya jana kabla ya kulimwa kadi ya njano dakika ya mwisho

Bao pekee la mchezo wa jana lilifungwa na beki Mbelgiji, Sebastien Dewaest dakika ya 49 akimalizia pasi ya kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero na ushindi huo unawapeleka nafasi ya pili kwenye ms... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More