SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUFUNGA MABAO MAWILI KRC GENK YASHINDA 3-1 UBELGIJI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUFUNGA MABAO MAWILI KRC GENK YASHINDA 3-1 UBELGIJI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameendelea kuisaidia timu yake, KRC Genk baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Sporting Charleroi kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji leo Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Samatta alifunga bao la pili dakika ya 77 na la tatu dakika ya 90 na ushei kwa penalti, baada ya beki Mfinland, Jere Uronen kufunga la kwanza dakika ya 45 na ushei, ambalo lilikuwa la kusawazisha kufuatia kiungo Mspaniola, Cristian Benavente kuanza kuifungia Sporting Charleroi dakika ya 27.
Na alifunga mabao hayo baada ya kuingia uwanjani akitokea benchi kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mbelgiji, Zinho Gano dakika ya 53.

Kwa ushindi huo, Genk inafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi nne na kupanda nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo, nyuma ya Anderlecht inayoongoza kwa pointi zake 12.
Samatta mwenye umri wa miaka 25, yupo katika mwaka wake wa tatu tangu asajiliwe Genk Januari 2... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More