SAMATTA AWAHOFIA MABEKI ‘MAGAIDI’ UBELGIJI MSIMU MPYA WA LIGI ZA ULAYA UKIKARIBIA KUANZA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAMATTA AWAHOFIA MABEKI ‘MAGAIDI’ UBELGIJI MSIMU MPYA WA LIGI ZA ULAYA UKIKARIBIA KUANZA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WAKATI msimu mpya wa Ligi mbalimbali Ulaya unakaribia kuanza, hofu kubwa ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji ni juu ya mabeki ‘magaidi’.
Ligi mbalimbali Ulaya na duniani kwa ujumla zinatarajiwa kuanz akuchezwa kuanzia Agosti baada ya kumalizika Mei mwaka huu.
Na Samatta ametumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea hisia zake kuelekea msimu ujao, akisema; “Muda wa kuanza kukimbizana na mabeki unakaribia, ila kuna mibeki mingine ina roho mbaya basi tu hakuna jinsi, muda wa kuanza kupasuka nao unakaribia,”.
Samatta ambaye ameposti picha akiwa na jezi mpya ya mechi za nyumbani na kuomba maoni ya mashabiki wake juu ya mwonekano wake, amesema kwamba msimu mpya unakaribia kuanza na wakati anafikiria kuanza kuwakimbiza mabeki, pia anafikiria kuumizwa na mabeki hao hao.

Mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta anawahofia mabeki ‘magaidi’ 

Samatta amekuwa na hofu na mabeki katili tangu a... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More