SAMUEL ETO'O KUZINDUA UWANJA WA SOKA OYSTERBAY JIJINI DAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAMUEL ETO'O KUZINDUA UWANJA WA SOKA OYSTERBAY JIJINI DAR


*kutua nchini Oktoba 10 mwaka huu.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

MCHEZAJI wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon na Barcelona Samuel Eto'o anatarajia kuja nchini  kwa ajili ya uzinduzi wa  mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira  wa soka  aina ya 5-A-side utakaojengwa Oysterbay jijini Dar es salaam.
Eto'o anakuja nchini kwa mualiko wa kampuni ya bia ya Tanzania (TBL) kupitia bia ya Castle Lager na atawasili Oktoba 10 mwaka huu.

 Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Meneja wa bia hiyo Pamela Kikuli amesema kuwa nyota huyo atashiriki katika uzinduzi  huo  wa uwanja maalumu wa soka linaloshirikisha wachezaji kumi (watano kila upande) maarufu kama ‘5-A-Side soccer’ katika eneo la Oysterbay  mkabala na jengo la Coco Plaza, jirani na fukwe za Coco.
 
Ameeleza kuwa lengo la kumleta nguli huyo wa soka barani Afrika ni kuongeza hamasa ya soka kwa wanamichezo wenye vipaji kujitokeza kushiriki katika kabumbu.
Pia amesema kuwa kama kampuni wataendelea kushiriki katika shughuli za kijamii kati... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More