SASA UKIAGIZA TIMU YA NJE KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NCHINI BILA RUHUSA YA TFF HAIFANYIKI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SASA UKIAGIZA TIMU YA NJE KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NCHINI BILA RUHUSA YA TFF HAIFANYIKI

Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), kupitia Mkugurugenzi wake wa Mashindano, Salum Madadi limezuia timu za nje ya nchi kuja kucheza mechi ya kirafiki au kushiriki mashindano mabalimbali nchini  bila kibali cha shirikisho hilo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Madadi amesema kwamba taratibu zilizowekwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) zinazosimamiwa na vyama vya soka vya nchi wanachama wake zinapaswa kueshimiwa.
Madadi, kocha wa zamani wa klabu mbalimbali na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema agizo hilo linawahusu wanachama wote wa shirikisho hilo ambao ni vyama vya soka vya mkoa, klabu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la kwanza, Ligi Daraja la Pili, Ligi Daraja la Tatu na wengineo.

Mkurugenzi huyo amesema wamelazimika kutoa onyo hilo baada ya matukio ya hivi karibuni ya kualikwa kwa timu za Kenya kuja kucheza mechi za kirafiki katika mikoa ya Dar es salaam na Mara bila kufuata taratibu za TFF kwa mujibu wa kanuni ya 15 ya... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More