SAVE THE CHILDREN WATIMIZA MIAKA 100, WAJA NA MKAKATI WA MIAKA MITATU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAVE THE CHILDREN WATIMIZA MIAKA 100, WAJA NA MKAKATI WA MIAKA MITATU

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv.
Shirika la Save the Children limesherehekea kutimiza kwa miaka 100 toka kuanzishwa kwake sambamba na kuzindua mkakati wa miaka mitatu wa kuwalinda na kuwajali watoto.
Mkakati huo unaoanzia mwaka 2019 hadi 2021 kwa ajili ya watoto Tanzania umewekwa kwenye vipengele saba ambazo zitaangaliwa changamoto zinazowakabili watoto nchini.
Akizungumzia mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watoto Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza amesema shirika la save the Children ni wadau wakubwa na wamekuwa wanashirikiana na serikali katika kusaidia na kuwalinda watoto.
Magwiza amesema, shirika hilo lipo nchini kwa miaka 38 na wanafanya kazi kulingana na mipango ya serikali kwa kuangalia namna gani wanawalinda watoto na wamekuwa wakiandaa mikakati mizuri inayomlinda mtoto.
Amesema, wamekuwa wanasaidia kutoa elimu rika kwa vijana waliobalehe, kuwawezesha watoto kielimu na kujitambua jambo ambalo limekuwa na msaada mkubwa sana kwa tai... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More